TAMISEMI YAMPONGEZA WAZIRI MKUU - CAPITAL TZ BLOG DODOMA

Latest

BANNER 728X90

Tuesday 24 November 2015

TAMISEMI YAMPONGEZA WAZIRI MKUU

index2Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Majaliwa Kassim Majaliwa akiongea na baadhi ya vingozi na watendaji wakuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) alipotembelea Wizara hiyo kwa lengo la kuongea viongozi hao kuhusu utendaji kazi wenye tija kwa wananchi leo jijini Dar es salaam.

index1Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) akitoa taarifa fupi kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Majaliwa Kassim Majaliwa alipotembelea Wizara hiyo leo jijini Dar es salaam.
……………………………………………………………………….
Na Shamimu Nyaki-Maelezo
Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) imempongeza Mhe. Majaliwa Kassimu Majaliwa kwa kuteuliwa kuwa Waziri Mkuu wa Kumi na Mmoja wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na kuahidi kushirikiana naye kwa karibu katika utekelezaji wa majukumu yake.
Akizungumza kwa niaba ya wafanyakazi wa (TAMISEMI),Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Jumanne Sagini amewaagiza watumishi katika wizara hiyo kufanya kazi kwa bidii kwa kuzingatia maadili ya kazi pamoja na kujiepusha na tabia ya uzembe, uvivu na wizi katika maeneo yao ya kazi.
Katika halfa hiyo iliyofanyika kwenye, Ofisi za TAMISEMI amewasilisha majukumu ya ofisi na muundo uliopo katika ofisi ikiwa ni pamoja na idara na taasisi zilizopo katika wizara hiyo zitakazo kuwa chini ya Waziri Mkuu huyo.
Aidha TAMISEMI imemuhakikishia Waziri Mkuu kuwa itafanya naye kazi kwa kasi kubwa kwa kuzingatia sheria na kanuni zilizopo katika ofisi hiyo ili kuleta mafanikio chanya ndani ya Serikali kwakuwa wizara hiyo ndio inayoshughulikia kwa kiasi kikubwa utekelezaji wa sera za maendeleo kwa wananchi.
Akizungumzia kuhusu hotuba ya Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli aliyoitoa Bungeni hivi karibuni, Katibu Mkuu huyo amewaambia waandishi wa habari kuwa watasimamia na kutekeleza yote yalioainishwa na Mhe. Rais hasa kuhusu suala la elimu ya sekondari na msingi kwakuwa wao ndio watendaji na wasimamizi katika sekta ya hiyo.
Hata hivyo ameziagiza halmashauri zote nchini kuhakikisha zinasimamia ujenzi wa nyumba za waalimu,madarasa pamoja na maabara kwakuwa wao ndio wenye mamlaka ya kusimamia suala hilo katika utekelezaji wake.
“Wakurugenzi wa halmashauri wao ndio watekelezaji wakuu wa katika kusimamia ujenzi wa madarasa,nyumba za waalimu zenye heshima kwa waalimu”alisema Katibu Mkuu Sagini.
Aliongeza kuwa ushirikiano miongoni mwa wanyafakazi katika ofisi hiyo utamuwezesha kutekeleza majukumu yake kwa urahisi na kasi kubwa katika kuwatumikia wananchi wa Tanzania.