KIBAKA ANUSURIKA KUFA KWA KUPORA SIMU DUKANI - CAPITAL TZ BLOG DODOMA

Latest

BANNER 728X90

Saturday, 15 November 2014

KIBAKA ANUSURIKA KUFA KWA KUPORA SIMU DUKANI

 Kijana ambaye hakuweza kufahamika jina lake mapema, akiugulia maumivu baada ya kupokea kichapo kutoka kwa wananchi wenye hasira kwa kile walichomtuhumu kuiba simu katika moja ya duka lililopoa maeneo ya Makumbusho karibu na Kituo cha Daladala, jijini Dar es Salaam. 
Wakielezea tukio hilo mashuhuda walisema kuwa kijana huyo aliingia katika duka hilo lililokuwa na mwanadada na kupora simu iliyokuwa juu ya kabati la bidhaa na kutimka nayo jambo lililomfanya mwanadada huyo kutoka nje na kuanza kupiga kelele za kuomba msaada.