UZINDUZI KAMPENI YA LISHE MKOA WA DODOMA (MWANZONI MWA WIKI HII) - CAPITAL TZ BLOG DODOMA

Latest

BANNER 728X90

Wednesday, 12 February 2014

UZINDUZI KAMPENI YA LISHE MKOA WA DODOMA (MWANZONI MWA WIKI HII)

Wakinamama wa wilaya ya Wilaya ya mpwapwa wakijipatia elimu ya lishe bora kwa mama na mtoto kwa njia ya vipeperushi wakati wa uzinduzi wa kampeni ya lishe mkoa wa Dodoma uliofanyika kimkoa wilayani mpwapwa mwanzoni mwa  wiki hii.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi akimnywesha uju wa lishe mtoto Devotha Samira ili kumwongezea virutubisho mwilini wakati wa uzinduzi wa kampeni ya lishe bora mkoa wa dodoma uliofanyika mwanzoni mwa wiki hii Wilayani mpwapwa, anayeshuhudia ni mama mzazi wa mtoto Devotha Bi. Marium Samira.


Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi akiwa kwenye picha ya pamoja na watoto Anthonia John (kushoto),Elizabeth Rafael (katikati) na Loy Juma waliopatiwa chakula dawa kwa ajili ya kuongeza virutubisho mwilini  ikiwa ni moja ya mazoezi yaliyofanywa kwenye uzinduzi wa kampeni ya lishe mkoa wa Dodoma uliofanyika mwanzoni mwa wiki hii wilayani mpwapwa.