Waziri
Mkuu Mstaafu Ndugu Edward Lowasa kizungumza na waandishi wa habari baada
ya kumaliza kuhojiwa na Kamati Ndogo ya Maadili kwenye Makao Makuu ya
Chama Cha Mapinduzi ambapo alisema mazungumzo yalikuwa mazuri,yalikuwa
yenye nia ya kukijenga chama kwa ajili ya uchaguzi 2015.
Kamati
Ndogo ya Maadili ya CCM inayoongozwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara)
Ndugu Phillip Mangula leo imewahoji watu watatu ambao wawili
walishawahi kuwa Mawaziri Wakuu katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano
ya Tanzania. Mawaziri hao waliohojiwa leno ni Waziri Mkuu Mstaafu Edward
Lowasa,Waziri Mkuu wa Zamani Ndugu Fredrick Sumaye na Mbunge wa
Sengerema Ndugu William Ngeleja ambaye pia alishawahi kuwa Waziri wa
Nishati na Madini.
Kamati
hiyo bado ina kazi ya kuwahoji viongozi wengine watatu ambao leo
walishindwa kufika baada ya kuomba udhuru kwani walikuwa na majukumu
mengine ya kiserikali, ambao hawajafika leo ni Waziri wa Mambo ya Nje
Ndugu Bernard Membe ambaye yupo safarini nje ya nchi ,Waziri wa Nchi
Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu) Ndugu Stephen Wassira na Naibu
Waziri wa Sayansi na Teknolojia Ndugu Januari Makamba.
|